“Uwepo wa ajira za Watanzania hususan watumishi wa bandari ya Dar es Salaam ni kipaumbele kikubwa cha Serikali sio tu katika Azimio hili bali katika kila aina ya uwekezaji ambao nchi itaufanya. Ibara ya 13 ya Mkataba huu inaitaka DP World kuendeleza ajira za watumishi wote waliopo, kuwaajiri Watanzania pamoja kuwaendeleza kitaaluma.
Vile vile Mkataba huu umeweka bayana sharti kwa Kampuni ya DP World kutumia Wakandarasi wa ndani katika manunuzi ya huduma na bidhaa pamoja na kusaidia Vyuo vya mafunzo vya Tanzania katika masuala ya elimu ya usafirishaji majini.”Waziri wa Uchukuzi Makame Mbarawa.