Akamatwa kwa kumiliki bastola kiholela

JESHI la polisi mkoani Shinyanga limefanikiwa kukamata bastola yenye namba 07IT4823 ikiwa na risasi tano katika doria iliyofanyika mwezi Mei hadi Juni 21 mwaka huu.

Risasi hizo na bastola zilipatikana kwenye begi moja lililokuwa limebebwa na watuhumiwa ambao walipakizana zaidi ya wawili kwenye pikipiki eneo la Msalala Wilaya Kahama na kuonekana kuwa na wasiwasi walipofatiliwa walitelekeza pikipiki na begi kisha kukimbia.

Kamanda wa polisi Mkoa Shinyanga, Janeth Magomi amesema hayo leo tarehe 21/Juni/2023 alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake huku akieleza licha ya kukamata bastola hiyo wamefanikiwa kukamata vitu mbalimbali ikiwemo kilo 60 na gramu 540 za bangi.

Kamanda Magomi alisema katika kipindi hicho wamefanikiwa kupeleka kesi moja ya mtuhumiwa wa mauaji Mahakamani naye hukumu imetoka kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa.

“Kuna kesi tatu za ubakaji ambayo moja mtuhumiwa alikutwa akijaribu kubaka ambapo imetolewa hukumu mahakamani kufungwa.

Habari Zifananazo

Back to top button