JESHI la polisi mkoani Geita linamshikilia, Simon Faida (24) mkazi wa Kijiji cha Msasa, Kata ya Busanda wilayani Geita kwa tuhuma za kumnajisi mtoto mwenye umri wa miaka nane.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Adam Maro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo mbele ya waandishi wa habari na kueleza mtuhumiwa ni kinyozi na alitenda ukatili huo Julai 23, 2023.
Ameeleza, aliyefanyiwa ukatili huo ni mwanafunzi (jina linahifadhiwa) na tukio liliripotiwa kituo cha polisi Julai 24, 2023 baada ya baba mzazi wa mtoto huyo, Mussa Kambona kubaini tatizo kwa mwanawe.
Amesema baba wa mtoto alibaini tatizo hilo baada ya kumuona mwanawe akipata shida kujisaidia, ndipo aliposhirikiana na mama wa mtoto kufanya uchunguzi na baadaye kufikisha taarifa polisi.
Comments are closed.