Akamatwa mauaji ya watu wawili Marekani

MTU mmoja aliyedhaniwa kuwa na bunduki nne amewauwa watu wawili na kuwajeruhi watano katika sherehe ya mahafali ya chuo kimoja iliyopo katika jiji la Richmond, Virginia, Marekani, polisi wamesema.

Polisi walisema walimkamata mtu mmoja, mwanaume mwenye umri wa miaka 19 jana karibu na jumba la maonyesho ambapo sherehe ya kuhitimu ilifanyika karibu na chuo kikuu cha Virginia Commonwealth.

Mshukiwa huyo huenda akashtakiwa kwa makosa mawili ya mauaji na makosa mengine, Mkuu wa Polisi wa Richmond, Rick Edwards amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari.

“Waliposikia milio ya risasi, ni wazi ilikuwa machafuko,” alisema. “Tulikuwa na mamia ya watu katika hifadhi ya Monroe, kwa hivyo watu walitawanyika.

Kulikuwa na fujo sana katika eneo la tukio.

Habari Zifananazo

Back to top button