Akinamama chanzo cha watoto kudumaa

DAR ES SALAAM: Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe (TFCN) Dk Germana Lyena amesema sababu kubwa ya udumavu wa watoto nchini ni wanawake kutumia muda mwingi kufanya kazi za uzalishaji kuliko kuwa na watoto wao.

Mikoa ya inayoongoza kwa udumavu nchini ni Iringa kwa asilimia 59.9, Njombe kwa asilimia 50.4 na Rukwa kwa asilimia 49.8, huku ripoti ya utafiti wa hali ya uzazi ya afya ya mama na mtoto na malaria inaonesha kuwa udumuavu umepungua nchini  hadi asilimia 30 mwaka 2022.

Akizungumza wakati akijibu maswali ya wabunge wa kamati ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI  amesema udumavu unatokea katika kipindi mtoto ni mdogo ambapo akinamama wengi siku hizi wanaingia katika shughuli za kiuchumi mapema kwahiyo hata malezi ya mtoto mdogo kuweza kuhakikisha amepewa chakula anachokihitaji ni mdogo.

Advertisement

“Mijini kuna rasilimali fedha kuweka dada ambaye atakaa na mtoto lakini vijijini hawana huo uwezo kwahiyo mtoto anaachwa nyumbani analelewa na mtoto mwenzake na kula viporo hilo ni sababu kubwa sana tumekuta katika maeneo mengi,”amesisitiza.

Amesema wanaendelea kufanya utafiti ambao bado haujakamilika unafanyika katika mikoa inayozalisha chakula  kwa wingi na yenye udumavu sana pamoja na mikoa ambayo imepunguza kwa kiasi kikubwa.

Amebainisha kuwa sababu kubwa ambayo wameiona inaeleza kuwa udumavu unasababishwa na malezi,makuzi ambapo muda wa kinamama na familia kulea watoto na kuhakikisha wanakula ipasavyo ni mdogo.

“Lakini bado kuna mikoa ambayo inamaambukizi makubwa ya maradhi ambayo tunajua inachangamoto za lishe kama Iringa ,Njombe,Mbeya,kuna kiwango kikubwa cha maambukizi ya UKIMWI inawezekana ni moja wapo ya sababu,”amefafanua Dk Lyena.

1 comments

Comments are closed.