Al Ahly kama Yanga tu!

MABINGWA wa muda wote wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) Al Alhy ya Misri imetinga hatua ya fainali kwa kuvuna jumla ya mabao 4-0, baada ya usiku wa kuamkia leo kushinda bao 1-0 katika uwanja wake wa  nyumbani dhidi ya Esperance De Tunis.

Idadi ya magoli ya kufuzu ya Al Ahly yanafanana na yale ya mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) Yanga, kwa kufuzu hatua ya fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) kwa kuvuna mabao manne kwa michezo ya nyumbani na ugenini dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini Mei 17, 2023.

Yanga ilishinda Dar es Salaam mabao 2-0, ikaenda kushinda ugenini mabao 2-1.

Hata hivyo, ilikujua watakutana nani mchezo wa fainali Al Ahly anasubiri matokeo ya mchezo wa marudiano leo nchini Afrika Kusini kati ya timu yenye kiwango bora CAFCL 2022/2023  Mamelodi Sundown dhidi ya Wydad Casablanca, waliotoka suluhu  walipokutana mechi ya mkondo wa kwanza nchini Morocco

Huku Yanga katika hatua ya fainali ya CAFCC 2022/2023 tayari ameshafahamu atakutana na USM Alger ya nchini Algeria waliofuzu kwa matokeo ya jumla 2-0 dhidi ya ASEC Mimosas.

Ambapo mechi ya mkondo wa kwanza itachezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam Mei 28, 2023 na mkondo wa pili kupigwa Juni 3, 2023 Uwanja wa Omar Hamad nchini Algeria

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button