KLABU ya Al-Ahly ya Misri imefika nchini usiku wa leo ikiwa ni maandalizi kuelekea mchezo wa African Football League dhidi ya Simba SC.
–
Mabingwa hao mara 11 wa Ligi ya Mabingwa Afrika, watacheza mchezo huo wa ufunguzi kesho Ijumaa katika uwanja wa Mkapa.
–
Ikumbukwe, timu hiyo itakutana na timu mbili kubwa za Tanzania kwenye michuano miwili mikubwa tofauti.
–
Itakutana na Yanga pia kwenye mchezo wa kundi D, linalojumuisha timu za Al-Ahly, Belouzdad na Medeama ya Ghana.


Add a comment