Al Hilal kukipiga na Simba SC

Klabu ya Al Hilal ya nchni Sudan itaweka kambi Tanzania kujiandaa na mchezo wao wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, ambapo ikiwa nchini itakipiga na Simba SC katika mchezo wa kirafiki.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 24, 2023, Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu amesema timu hizo zitashirikiana katika maeneo saba ikiwa ni pamoja na kutembeleana na kubadilishana uzoefu.

Al Hilal watawasili Januari 25, 2023 watacheza mchezo wa kwanza Januari 26, 2023 dhidi ya Namungo, mchezo wa pili utapigwa Januari 31 dhidi ya Azam FC, katika Uwanja wa Azam Complex.

Februari 5, 2023 watacheza na Simba SC katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, na baada ya hapo Februari 6 itaondoka kuelekea na Afrika Kusini tayari kuikabilia Mamelodi Februari 11.

Al Hilal imepangwa katika Kundi B pamoja na Al Ahly, Coton Sport na Mamelod Sundowns, wakati wenyeji wao Simba wamepangwa na timu za Horoya, Raja Club Athletic na Vipers.

Habari Zifananazo

Back to top button