ALAF yasaidia mabati 269 ujenzi wa madarasa Newala

KAMPUNI ya uzalishaji wa mabati ya ALAF, imetoa msaada wa mabati 269 kwa Halmshauri ya Newala, mkoani Mtwara.

Mabati hayo yametolewa kupitia ofisi ya Mbunge, Jimbo la Newala Mjini kwa ajili ya kuwezeka kwenye majengo mapya yanayojengwa katika shule za sekondari na msingi katika halmshauri hiyo.

Waziri wa nchi Ofisi ya Raisi (Kazi Maalumu), George Mkuchika, ambaye ni Mbunge wa Newala Mjini, ameushukuru uongozi wa ALAF kwa kuunga mkono serikali kwenye maendeleo ya elimu Newala.

Akitoa taarifa kuhusu msaada huo katika hafla ya makabidhiano ya mabati hayo, Kaimu Mkurungezi wa halmshauri hiyo, George Musa amesema mabatii hayo yatatumika kuezeka majengo baadhi ya shule, ikiwemo shule mpya ya Chiunchijila Mto Ruvuma, ambayo inajengwa kwa mapato ya ndani.

Meneja Kitengo cha Uhusiano ALAF, Hawa Bayumi, amesema msaada huo wameutoa kwa ajili ya kuunga mkono serikali katika kuendeleza masuala ya elimu haswa kwenye upande wa watoto wa kike.

“Ni furaha yetu kuona tunaisaidia serikali katika jitihada zake ambazo inafanya hasa kwenye suala la elimu,” amesema na kumshukuru Waziri Mkuchika kwa kuona ALAF kama wadau muhimu katika kusaidia serikali kwenye maendeleo.

Habari Zifananazo

Back to top button