ALAT Katavi yatoa neno suala la vitega uchumi

JUMUIYA ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT), Mkoa wa Katavi, imewaomba wakurugenzi watendaji wa Halmashauri tano za Mkoa huo kutenga fedha, kupitia bajeti ya mwaka ujao.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa maazimio ya vikao vyao kwamba ALAT inatakiwa kuwa na vitega uchumi vyake, ili kujiendesha.

Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Katavi, ambaye pia ni Meya wa Manispaa ya Mpanda, Haidary Sumry, wakati akihitimisha kikao cha kawaida cha ALAT Mkoa wa Katavi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Mpanda.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa ALAT, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tanganyika, Hamad Mapengo, ametoa wito kwa wakurugenzi kutekeleza maazimio ya vikao kwa kuhakikisha kila halmashauri inatenga fedha za uanzishaji vitega uchumi kwa mujibu wa makubaliano.

Naye Soud Mbogo, Diwani wa Kata ya Inyonga na Mwenyeketi wa halmshauri ya Mlele, amesema kuwepo kwa vitega uchumi vya ALAT Mkoa kutawarahisishia kutekeleza baadhi ya mambo pasipokusubiria michango kutoka katika Halmashauri.

 

Habari Zifananazo

Back to top button