Algeria kuwekeza kwenye Mkonge nchini

BODI Mkonge Tanzania (TSB) imefanya mazungumzo na wawekezaji kutoka Algeria ambao wameonyesha nia ya kuwekeza kwenye Mkonge.

Bodi imekutanishwa na wawekezaji hao kupitia Kituo cha Uwekezaji (TIC) na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade)

Akizungumza na HabariLeo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ‘Sabasaba 2023’ Mkurugenzi Mkuu wa TSB, Saddy Kambona amesema  wamezungumza  mambo mbalimbali lakini kubwa zaidi ni kwamba wana nia ya kuwekeza, kulima na kununua Mkonge kutoka hapa nchini.

Advertisement

“Tumekubaliana hivi karibuni tutawapeleka kutembelea mashamba ya Mkonge ili kujionea uzalishaji, uwekezaji na fursa zilizopo,” amesema Kambona.

Amesema, TSB imekuwa na utaratibu wa kuhamasisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kuwekeza kwenye sekta ya Mkonge ambayo inaendelea kukua siku hadi siku.

3 comments

Comments are closed.