Aliyeiba mtoto atiwa mbaroni

JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa wizi wa mtoto.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa alisema hayo jijini hapa wakati wa mahojiano na gazeti hili jana.

“Machi 26 muda wa saa 08:00 asubuhi katika Mtaa wa Migombani, Kata ya Nyampulukano, Tarafa ya Sengerema, kuliripotiwa taarifa ya wizi wa mtoto

aitwaye Anitha Richard mwenye umri wa miezi 6 na mtu ambaye hakujulikana,” alisema Kamanda Mutafungwa.

Alisema baada ya kuripotiwa kwa tukio hilo, askari polisi walifanya msako mkali na kufika katika Kijiji cha Nyamaduke na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa, Happyness William ambaye ni mkulima na mkazi wa Nyehunge akiwa na mtoto huyo aliyetambuliwa na wazazi wake.

Kamanda Mutafungwa alisema baada ya mahojiano na mtuhumiwa alikiri kuhusika na tukio la wizi wa mtoto huyo ambapo alidai kuwa alienda kumwonesha mumewe kuwa amejifungua.

Alisema upelelezi wa kesi hiyo umekamilishwa mara moja na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kukabiliana na mkono wa sheria.

 

Habari Zifananazo

Back to top button