Aliyekosa fedha za kujikimu apora, afungwa miaka 30

MWANZA: John Chibuga (31) mkazi wa Kijiji cha Bugolola wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la  unyang’anyi wa kutumia silaha.

Hukumu hiyo imetolewa jana Februari 23.2024 na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Ukerewe, Lucas Nyahega ambapo amesema kupitia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, Mahakama imejiridhisha pasi na shaka kwamba mshtakiwa ametenda kosa hilo.

Hata hivyo, mshitakiwa alipopewa nafasi ya kujitetea ili apunguziwe adhabu kutokana na shitaka linalomkabili,aliomba mahakama impunguzia adhabu kwa sababu alikuwa hana pesa ya kujikimu baada ya kutoka gerezani ndio akaamua kwenda kupora.

Aidha, Mwendesha mashtaka aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa ni mtenda kosa wa mara ya pili na aliachiliwa huru kwa msamaha wa  Rais Desemba 09, 2023 kwa kosa la Kuvunja dukauUsiku na kuiba.

 

Habari Zifananazo

Back to top button