Aliyekuwa mwenyekiti Simba afariki dunia

SIMBA SC imetangaza kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Ayubu Saleh Chamshama aliyefariki Agosti 11, 2023 akiwa hospitali nchini India.

Taarifa ya klabu hiyo imeeleza kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Soud Chamshama msiba utakuwa nyumbani kwake Chang’ombe Maduka Mawili.

Aidha, mazishi yatafanyika kesho kijiji cha Kilole Lushoto mkoani Tanga.

Uongozi wa Simba umetoa pole kwa ndugu, jamii na marafiki walioguswa na msiba.

Habari Zifananazo

Back to top button