Aliyembusu mchezaji afungiwa miaka mitatu

RAIS wa zamani wa Chama cha Soka Uhispania (RFEF), Luis Rubiales amepigwa marufuku kujihusisha na soka kwa miaka mitatu.


Agosti 26, 2023 Luis Rubiales alisimamishwa kujihusisha na soka kwa siku 90 na Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) kupisha uchunguzi kuhusu kumbusu mchezaji wa Uhispania, Jenni Hermoso wakati ugawaji medali fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake.

Rubiales alimbusu mchezaji huyo midomoni wakati wa hafla ya utoaji tuzo huko Sydney mnamo Agosti 20. Pia alimbeba Athenea del Castillo begani wakati wa sherehe za ushindi wa bao 1-0 dhidi ya England.

Advertisement

Wakati Rubiales mwanzoni alijaribu kuendelea na jukumu lake, alijiuzulu kuwa Rais wa RFEF na Makamu wa Rais wa UEFA mwezi uliopita, na sasa ameadhibiwa kwa kukiuka kifungu cha 13 cha kanuni za nidhamu za FIFA.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *