Aliyemkata kiganja mkewe jela miaka 4

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha, imemhukumu kifungo cha miaka minne jela  aliyekuwa mtumishi wa Shirikala UmemeTanzania (Tanesco), Ombeni Alfayo na kumwamuru kumlipa fidia ya Sh Milioni 15 mke wake Veronica Kidemi (30) baada ya kukutwa na hatia ya kosa la kujaribu kuua.

Alfayo ambaye alimkata mke wake na sime kiganja cha mkono wake wa kulia kwa wivu wa mapenzi, amepata hukumu hiyo  leo mbele ya  Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Arusha, Joachim Tiganga, ambapo Jaji huyo amesema mahakama imeamua kupunguza adhabu ya hukumu hiyo baada ya mshtakiwa kukiri mahakamani kutenda kosa hilo na hana rekodi nyingine ya uhalifu.

Akinukuu hukumu mbalimbali zilizotolewa na mahakama nyingine tofauti, Jaji Tiganga alisema kosa alilofanya kifungo cha maisha jela, lakini kwa kua mshtakiwa hana rekodi za kushtakiwa na ni kosa lake la kwanza, lakini pia ana watoto wawili kwa mke wake mahakama imeona ni heri kumpunguzia adhabu hiyo.

Veronica ambaye ni mke wa mshitakiwa Ombeni Alfayo akifuatilia hukumu mahakamani leo.

Jaji Tiganga alisema kwa kuwa shtaka lake ni la kujaribu kuua chini ya kifungu namba 211 cha sheria ,hivyo mahakama hiyo imezingatia kosa alilolofanya pamoja na shufaa alizozitoa mahakamani hapo wakati wa kujitetea.

“Kosa ulilofanya lilistahiki ufungwe maisha na kwakua hujasumbua mahakama ulikiri kosa nakuhukumu miaka minne jela na fidia ya sh Milioni 15 umpe mkeo, ili kupunguza machungu aliyopata na ushahidi wako uliomba usipewe adhabu kubwa sababu una watoto, ” alisema.

 

Habari Zifananazo

Back to top button