Aliyesababisha ajali Mwanza akamatwa

Jeshi la polisi mkoani Mwanza limemkamata Oswald Kaijage Binamungu (39) mhandisi wa umeme katika mgodi wa Geita Gold Mining (GGM) mkazi wa Buswelu Manispaa ya Ilemela aliyetoroka baada ya kusababisha ajali eneo la Lumala iliyopelekea vifo vya watu sita na kujeruhi 16 Julai 22, 2023.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani hapa, Wilbroard Mutafungwa amesema kuwa ajali hiyo ilihusisha gari lenye namba za usajili T.476 DZL aina ya Toyota Hilux Double Cabin iliwagonga watu waliokua wakifanya mazoezi kando ya barabara.
 
Mutafungwa ameeleza baadhi ya majeruhi waliokuwa wanatibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure wameruhusiwa kurudi nyumbani huku wanne wakibaki kwa matibabu na watano wakiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.
 
Aidha katika hatua nyingine kamanda Mutafungwa amevikumbusha vikundi vya ‘jogging’ kusajili vikundi vyao kwenye ofisi za utamaduni katika ngazi za wilaya, manispaa na jiji ambapo watapewa miongozo au maelekezo ya namna bora ya kufanya mazoezi kwa kuzingatia hali ya usalama wao na watu wengine.

Habari Zifananazo

6 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button