MWANAMKE aliyeshiriki katika historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ya kuchanganya udongo, Khadija Abbas Rashid amefariki dunia akiwa na miaka 74.
Kaimu Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, Hanifa Selengu amethibitisha leo Agosti 22, 2023 kifo hicho.
Kwa upande wake, binti wa marehemu Aziza Makarani akielezea msiba huo amesema mama yake amefariki leo Jumanne majira ya 8:30 mchana akiwa nyumbani kwao Rahaleo katika Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.
Marehemu alikuwa miongoni mwa walioshiriki katika sherehe ya mfano ya kuchanganya udongo kutoka Tanganyika na Zanzibar , Aprili 26 mwaka 1964.