Aliyetorosha mtoto, kumbaka kuozea jela

Afungwa jela maisha kwa kulawiti hadharani

MAHAKAMA ya Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu imemhukumu Kulwa Meleka kifungo cha miaka 70 jela na kulipa faini ya Sh milioni moja baada ya kumtia hatiani kwa makosa ya kumtorosha binti mwenye umri wa miaka 13 na kumbaka.

Mfungwa huyo mpya, mkazi wa Kata ya Nkololo, wilayani Bariadi anadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Novemba mwaka jana hadi Machi mwaka huu.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Caroline Kiliwa baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Advertisement

Kabla ya Kulwa kusomewa adhabu, Wakili wa Serikali, Vailet Mshumbushi aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa Kulwa.

Akisoma hukumu, Caroline alisema kwa kosa la kwanza la kumtorosha mtoto huyo anamhukumu kifungo cha miaka 10 na kosa la pili la kumpeleka sehemu isiyojulikana miaka 30 huku kosa la tatu la kubaka akitakiwa pia kutumikia kifungo cha miaka 30 jela. Kulwa anatakiwa pia kulipa faini ya Sh milioni moja.

 

 

 

 

d

/* */