Aliyeua mlinzi wa kanisa ahukumiwa kunyongwa

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu kunyongwa mpaka kufa mkazi wa Dar es Salaam, Omari Juma baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumuua kwa kukusudia aliyekuwa mlinzi wa Kanisa la Moravian Tabata Segerea, Timoth Kyage.

Aidha, mahakama hiyo imemuachia huru Ramadhani Omari baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake katika kesi hiyo.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa hukumu.

Katika maelezo ya hukumu hiyo ilielezwa kuwa Agosti 21, 2017, Omari pamoja na wenzake watatu waliruka ukuta wa kanisa hilo na kumvamia Timoth kisha kumfunga mdomo na pua kwa plasta ili asipige kelele na kumfunga miguu na mikono kutumia kamba za katani kisha kumpiga na kumjeruhi vibaya.

Akisoma hukumu hiyo, Pamela alisema kuwa wakati wa uendeshwaji wa kesi hiyo mshtakiwa huyo alikiri kosa na kuieleza mahakama kuwa walivamia kanisa hilo baada ya kupewa taarifa na rafiki yake kuwa kulikuwa na fedha ndani ya kanisa hilo hivyo waliingia kwa ajili ya kuziiba japo hawakuzikuta.

Wakati tukio hilo likiendelea mlinzi wa kanisa la jirani ambalo ni Kanisa Katoliki aligundua kuwa kuna uvamizi unaendelea kanisani hapo kisha kupiga risasi angani jambo lililowafanya wahalifu watatu kukimbia na alibaki Omari aliyeshindwa kukimbia baada ya kudhibitiwa.

Uchunguzi wa daktari ulionesha kuwa marehemu alipigwa na kitu kizito katika sehemu ya kichwa chake kiasi cha kupelekea ubongo kuonekana pia alikosa hewa kutokana na kuzibwa pua na mdomo hali iliyompelekea kupoteza maisha.

Katika kesi hiyo upande wa mashtaka ulileta mashahidi sita na vielelezo vinne ikiwemo ripoti ya uchunguzi wa mwili na ramani ya tukio.

Upande wa utetezi wakiongozwa na wakili Felix Mutaki uliiomba mahakama kuwapunguzia washtakiwa adhabu kwani lilikuwa kosa lao la kwanza kulitenda.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Kim
Kim
2 months ago

I am now making $19k or more every month from home by doing very simple and easy job online from home. I have received exactly $20845 last month from this home job. Join now this job and start making cash online by

Follow instruction on website Here. . . . . . . .>>> http://www.Richcash1.com

Last edited 2 months ago by Kim
Ansarra
Ansarra
2 months ago

!!!! Welcome to the best sex dating site — https://ok.me/wqPA1

Dawn K. Walker
Dawn K. Walker
Reply to  Ansarra
2 months ago

Given that I was unemployed a year ago as a result of the terrible economy, it is amazing that I run a home-based business and make a healthy $60k each week. It is now my duty to promote goodwill and make these instructions tn-32 available to others after being gifted with them.
.
.
Detail Here————————— https://Fastinccome.blogspot.com/

Julia
Julia
2 months ago

Earn income while simply working online. Work from home whenever you want. Just for maximum 5 hours a day you can make more than $600 per day online. From this I made $18,000 last month in my spare time.
.
.
Detail Here—————————————————————->>> http://Www.OnlineCash1.Com

Back to top button
4
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x