Aliyeua mtoto wa mkewe kisa ARVs kunyongwa

Wanne kunyongwa kwa kumuua diwani

MAHAKAMA kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora, imetoa hukumu ya kunyongwa hadi kufa Haruna Ndayanze baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mtoto wa mkewe kwa madai kuwa alimkuta mama yake akimeza vidonge vya kufubaza virusi vya Ukimwi (ARVS).

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Tabora, Demetrio Nyakunga alitoa hukumu hiyo baada ya kukasimiwa mamlaka ya kusikiliza mashauri ya mahakama kuu.

Nyakunga alisema mahakama hiyo imeridhika na ushaidi uliotolewa mahakamani hapo na hivyo mshitakiwa Ndayanze ametiwa hatiani kwa kumuua Kusaga Magulu ambaye ni mtoto wa mkewe aliyezaa na mwanaume mwingine.

Advertisement

Upande wa mashitaka ukiwakilishwa na mawakili, Merito Ukongoji na Sabrina Silayo ulidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Januari 25 mwaka 2020 katika Kijiji cha Pozamoyo wilayani Kaliua.

Ilidaiwa kuwa siku hiyo mshitakiwa ilimuua mtoto huyo kwa kumkata kwa panga shingoni, mikononi na sehemu nyingine za mwili.

Upande wa mashitaka ulipeleka mashahidi 12 na ukadai mahakamani kuwa sababu za mauaji hayo ni mshitakiwa kumkuta mkewe, Stephania Alphoncy akimeza ARVs.

Hakimu Nyakunga pia aliwahukumu kunyongwa hadi kufa, Ally Shaban Kinyogoli na Ally Mtoni Kambongo baada ya kuwakuta na hatia ya kumuua Ally Rajabu, mkazi wa Kijiji cha Igalula wilayani Uyui.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *