Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la kujenga Taifa JKT Julai 10, 2023 katika uwanja wa CCM Jamhuri jijini Dodoma
Akitoa Taarifa kwa vyombo vya habari Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa JKT, Innocent Bashungwa amesema maadhimsho hayo yatapambwa na gwaride la vijana wa jeshi la kujenga Taifa, maonyesho ya vifaa mbalimbali vya Sumajkt pamoja burudani za ngoma kutoka kwa vijana wa JKT