Amtoboa jicho mkewe wivu wa mapenzi

MWANAMKE mmoja Jackline Mnkonyi mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa Sombetini jijini Arusha amekutana na kipigo kutoka kwa mume wake, Isaac Mnyagi na kung’olewa meno mawili pamoja na kutobolewa jicho kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwa wazazi wake eneo la Sinoni Kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha ,Jackline alisema baada ya kupata kipigo hicho alichukuliwa bila kujitambua na kupelekwa nyumbani kwa wazazi wake Sinoni na kutupwa getini.

Alisema raia waliomfahamu ndio walimtambua na kuwapigia simu wazazi wake na walipofungua geti waliamua kumchukua na asubuhi alipelekwa hospital kwa matibabu.

Akizungumzia mkasa huo alisema mchana wa Mei 23, 2023 alitembelewa na mjomba wake ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu Vicenti Nicodemas.

Jackline alisema na kumtaja mume wake kwa jina la Isaack Mnyagi mwalimu na mkazi wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro huja baada ya muda wa zaidi ya miezi mitatu na zaidi kuona watoto wawili aliozaa nao na siku hiyo alikuja usiku ghafla.

Alisema alipofika nyumbani Sombetini majira ya saa 4.45 usiku aligonga mlango na kufunguliwa na watoto lakini hakutaka salamu na kuingia chumbani na alipomfuata alitoka.

Jackline alipoona hivyo alimuuliza kulikoni alichoambulia ni maneno mazito na matusi na kuulizwa mchana alikuwa na nani na alimjibu kuwa alikuwa na mjomba wake hatua ambayo alikana na kusema kuwa ni mtu wake na huwa wanafanya mapenzi hatua ambayo alipinga lakini alijikutaja akipigwa na ‘’mjeledi’’ mgongoni.

Alisema alijitahidi kujieleza lakini ilishindikana na mume wake alichukua ‘Plaizi’ kifaa cha gereji na kumwamuru afungue mdomo na kung’olewa meno huku akipata kipigo kikali na kujikuta na maumivu makali hadi.

Jackline alisema hatua hiyo aliona kama haitoshi aliamua kuchukua kitu chenye ncha kali na kumtoboa jicho moja ambalo hadi sasa hawezi kuona.

Alisema hakujua jinsi alivyofikishwa nyumbani kwa wazazi wake Sinoni na kutupwa getini kwani alishituka akiwa hospitali.

‘’Nimetobolewa jicho na nimeng’olewa meno mawili kwa chombo kinachoitwa Plaiz nina maamuvi makali sana naiomba serikali ichukue hatua dhidi ya mume wake kwani amenifanyia unyama wa hali ya juu’’alisema Jackline

Mzazi wa Jackline, Elimilis Mkonyi alisema kuwa baada ya kumpeleka katika Hospital ya Rufaa ya Mount Meru na kupata matibabu alikwenda kituo kikuu cha polisi Arusha na kufungua jalada shambuli la kuzulu mwili kesi namba ARS/RB/5416/2023.

Mkonyi mwenye watoto wanane na wajukuuu 16 alisema kuwa mume wa mtoto wake hamjui na hajawahi kujitambulisha kwake kwa muda wote waliofanikiwa kupata watoto wao wawili labda mama maana wao ndio wenye siri juu ya mahusiano hayo.

Alisema kuwa mtoto wake, Jckline aliwahi kumweleza mama yake kuwa mume wake amekuwa na tabia ya kumpiga mara kwa mara lakini yeye hajawahi kuelezwa kwani mtoto wa kike huongea zaidi na mama na hadi sasa hajulikani alipo mara baada ya kufanya tukio hilo la kinyama kwa jamii.

”Niliwahi kumzuia mwanangu asidi tena kwa mume wake lakini hakusikia kwani yeye mtoto na mama yake ndio wasiri wakubwa wa kila kitu kifupi naweza kusema hivyo tu mengine tuiache serikali ifanye kazi yake” alisema Mkonyi.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Justin Msejo hakuweza kupatikana kwa simu yake ya kiganjani kuelezea tukio hilo kama mtuhumiwa ameshakamatwa au la kwani  simu yake ya kiganjani ilikuwa ikiita bila kupokelewa. Tutaendelea kukupa taarifa zaidi.

Habari Zifananazo

Back to top button