Amzika mwanawe akiwa hai apate ‘kudanga’

JESHI la Polisi mkoani Geita linamshikilia Oliver Meshack (19), mkazi wa kitongoji cha Mapinduzi, kata ya Buselesele wilayani Chato kwa tuhuma za kumzika mwanawe akiwa hai, ili apate nafasi ya kuhangaika na wanaume kwa masuala ya ngono (kudanga).

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Safia Jongo ametoa taarifa hiyo leo alipozungumuza na waandishi wa habari ofisini kwake na kumtaja mtoto aliyezikwa alijulikana kwa jina moja la Queen akiwa na umri wa wiki mbili.

Kamanda amesema mtuhumiwa alitenda ukatili huo Desemba 2, 2022, majira ya saa nane usiku, ambapo taarifa zilifikishwa kituo cha polisi Desemba 6 na wananchi walidai kushangazwa na kupotea ghafla kwa kichanga huyo.

“Walisema wanajua kuna binti amejifungua mtoto, lakini wana siku zaidi ya tatu hawamuoni huyu binti akiwa na huyo mtoto, kwa hiyo wana wasiwasi na wanatamani wajue huyo binti amepeleka wapi huyo mtoto.

“Jeshi la polisi lilimchukua huyo binti na kufanya naye mahojiano, ambapo alikiri kwamba ni kweli alijifungua huyo mtoto ambaye alimzika akiwa na umri wa wiki mbili,” amesema na kuongeza:

“Kutokana na yeye kazi yake ni kuuza baa na pia anajiuza mwili wake, kwa hiyo yule mtoto akawa ni kero kwake, akawa anashindwa kwenda kufanya biashara yake hivo akaamua kuchimba shimo, na kumfukia huyo mtoto akiwa hai.”

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button