Andengenye anogesha tamasha la mlipa kodi Kigoma

KIGOMA: MKUU wa Mkoa Kigoma, Thobias Andengenye amefanikisha tamasha la michezo la kuhamasha ulipaji kodi kwa hiari akisema kuwa ulipaji kodi kwa hiari unafaida kubwa katika kuiwezesha serikali kuwa na mapato ya kutosha kugharamia mipango yake ya maendeleo ikiwemo michezo.

Tamasha hilo lililofanyika kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre mjini kwa uratibu wa Mamlaka ya mapato (TRA) Mkoa wa Kigoma likiwa na ujumbe wa shukrani kwa mlipa kodi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Kigoma, Mkuu wa Wilaya Kigoma, Salum Kali alisema kuwa serikali itasimamia kwa karibu kuwakamata na kuwachukulia hatua wafanyabiashara wote wanaoingiza bidhaa nchi kwa njia za magendo.

Kwa upande wa Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Mcha Hassan alisema kuwa mikutano na mabonza wanayofanya imekuwa na faida kubwa kutokana na kuongezeka maradufu kwa wigo wa walipa kodi lakini pia watu wengi wamekuwa wakipata elimu na hamasa ambayo imesaidia kukabili changamoto mbalimbali za kikodi kwenye biashara zao.

Katika bonanza hilo timu ya walipa kodi wafanyabiashara wa manispaa ya Kigoma Ujiji walifanikiwa kuwa mabingwa katika mpira wa miguu huku wafanyakazi wa TRA wakiibuka na ushindi wa kuvuta Kamba.

 

Habari Zifananazo

Back to top button