MWIMBAJI wa bongo fleva, Angelina George maarufu kama ‘Angela’ amewataka mashabiki wake kuwa na subira muda utakapofika kila kitu kitakuwa bayana.
Akizungumza na HABARILEO kwa njia ya simu, Angella aliomba kupewa muda kidogo aweke vitu sawa na baada ya hapo kila kitu atakiweka wazi kwa mashabiki zake na watanzania.
Anjella ameeleza hilo kufuatia mashabiki wake kutamani kujua hatma yake baada ya kuachana na Konde Gang hivi karibuni.