Nyota wa mpira wa kikapu wa Milwaukee Bucks , Giannis Antetokounmpo kwa mara ya kwanza amefunga pointi 55 za juu katika historia yake ya mchezo huo wakati timu yake ikipata ushindi wa pointi 123-113 dhidi ya Washington Wizards jana.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 pia alirekodi ya rebounds 10 na asisti saba na kumaliza mbio za ushindi wa mechi tano za Wizards.
Ilikuwa ni mara ya nne katika maisha yake ya soka kwa Antetokounmpo kufunga zaidi ya pointi 50 katika mchezo mmoja.
“Ninafanya kazi kwa bidii. Watu wengi wanadhani mchezo wangu unachosha, lakini ninafanya kila kitu kuboresha,” alisema.
Antetokounmpo mwenye asili ya Nigeria na Ugiriki ambaye amewahi kushinda tuzo ya MVP mara, aliongeza: “Nilijaribu kufanya maamuzi sahihi, kuongeza makali yangu nilifanya kila kitu kuhakikisha timu yangu inashinda.”
Katika mchezo huyo mchezaji mwenzake, Bobby Portis aliingia akitokea benchi na kufunga pointi 17 na rebounds 13. Pia siku ya Jumanne, Sacramento Kings waliwashinda Utah Jazz 117-115 katika mchezo mkali katika Jiji la Salt Lake.