Apigwa risasi akidhaniwa sungura

MTU mmoja nchini China amefariki baada ya kupigwa risasi na mwindaji akidhaniwa kuwa sungura.

Watu wanne wamekamatwa kutokana na kifo cha Wang Moujin, ambaye alianguka kwenye shimo baada ya kupigwa risasi kichwani.

Tukio hilo ni la juzi wakati watu hao wanne walipokwenda kuwinda katika Mji wa Shaxi, Mkoa wa Jiangxi. Matukio yanayohusisha bunduki ni nadra nchini China.

Polisi kutoka Wilaya ya Xinzhou walisema mmoja wa watu hao alifyatua risasi baada ya kuona kitu kikisogea kwenye nyasi kando ya mtaro. Inasadikiwa Wang alikuwa akivua samaki.

Baada ya tukio hilo, polisi waliitwa na kuwakamata watuhumiwa ambao ni wanaume wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 30.

Uchunguzi ulibaini kuwa pamoja na kwamba Wang alipigwa risasi, lakini alikufa maji baada ya kuzama mtoni.

 

Habari Zifananazo

Back to top button