OFISA wa ngazi ya juu wa Ukraine, ametaja uchunguzi wa Urusi kuhusu mlipuko wa juma lililopita ni “upuuzi.
”
Mlipuko huo uliharibu vibaya daraja linalounganisha Urusi na peninsula ya Crimea, ambayo Moscow iliinyakua kutoka Ukraine mwaka 2014.
Rais wa Urusi, Vladimir Putin, amevilaumu vikosi vya usalama vya Ukraine kwa mlipuko huo, mapema leo Idara ya Usalama ya Shirikisho la Urusi (FSB), ilisema imewashikilia Warusi watano na raia watatu wa Ukraine na Armenia kutokana na mlipuko huo.
“Shughuli nzima ya FSB na Kamati ya Uchunguzi ni upuuzi,” shirika la utangazaji la umma la Ukraine Suspilne lilimnukuu msemaji wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Andriy Yusov, akisema alipoulizwa kuhusu madai ya Moscow juu ya mlipuko wa Daraja la Crimea.