Apple yapigwa faini kwa kukiuka sheria EU

Apple

KAMPUNI ya teknolojia ya nchini Marekani ‘Apple’ imetozwa faini ya €1.8bn baada kukiuka sheria za Umoja wa Ulaya ‘EU’.

Imeelezwa kuwa uchunguzi umebaini ‘Apple’ ilikuwa na ushindani mdogo kutoka kwa huduma za utiririshaji muziki kama vile Spotify.

Faini hiyo ni mara nne zaidi ya ilivyotarajiwa katika hatua ya Tume ya Ulaya kuonesha itashughulikia kwa dhati kampuni za teknolojia zinazotumia vibaya nafasi zao kuu katika soko la simu na huduma za mtandaoni.

Advertisement

Makamu wa Rais Mtendaji wa Tume ya Ulaya, Margrethe Vestager alizionya kampuni zingene zenye kuhusu ukikwaji wa sheria.

“Nadhani ni muhimu kuona kwamba ikiwa wewe ni kampuni inayoongoza na ukifanya kitu kisicho halali, itaadhibiwa. Tunataka kuonesha azimio letu kwamba tutaingia katika kesi hizi,” Vestager alisema.