Arafat wa Yanga, Mkurugenzi mpya PBZ

ZANZIBAR: RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wa Serikali na Mashirika ya Umma yaliyo chini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi

Katika taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Zanzibar, Mhandisi Zena A. Said imetanabahisha kuwa Arafat Ally Haji ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ). Kabla ya uteuzi huo Arafat alikuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) pia ni Makamu wa Rais wa Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam.

Amemteua, Balozi Omar Yussuf Mzee kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Balozi Omar ni Mstaafu katika Utumishi wa Umma.

Pia, Dk Huda Ahmed Yussuf ameteuliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF

Naye, Saleh Saad Mohamed ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar ZIPA, kabla ya uteuzi huo, Saleh alikuwa Msaidizi Mkurugenzi Huduma za Uwekezaji ZIPA.

Dk Haji Gora Haji ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kitaifa na Uratibu wa Diaspora katika Ofisi ya Rais Ikulu. Kabla ya uteuzi Dk Haji alikuwa Mkuu wa Divisheni ya Mipango, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.

Taarifa hiyo ya Katibu Kiongozi imefafanua kuwa, uteuzi huo unaanza leo Mei 09, 2024.

 

Habari Zifananazo

Back to top button