Arsenal kuivaa Bayern, Man City dhidi ya Madrid

ARSENAL imepangwa kucheza na Bayern Munich robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku Manchester City ikipangwa na Real Madrid.

Droo iliyotolewa muda huu na Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA) imeonesha Barcelona itavaana na Paris Saint Germain.

Borrusia Dortmund itacheza na Atletico Madrid.

Michezo ya robo fainali itaanza Aprili 9, 2024. Raundi ya pili itachezwa Aprili 16/17.

Nusu fainali itapigwa Aprili 30, 2024 na Mei 7/8 itapigwa michezo ya marudiano.

Mchezo wa fainali utapigwa London, Juni 1, 2024.

Habari Zifananazo

Back to top button