Arsenal kupeleka dau la tatu kwa Rice

ARSENAL inajiandaa kuwasilisha ofa ya tatu kwa West Ham United baada ya mbili kukataliwa kuhusu usajili wa Declan Rice. Mtandao wa Mail umeripoti.

Awali Arsenal ilipelekea dau la Pauni milioni 10 kwa ajili ya usajili wa Rice, ‘The Hammers’ walikataa, jana ‘The Gunners’ walipeleka pauni milioni 90 ilikataliwa tena.

Arsenal bado inaendelea kuangalia uwezekano wa kupata saini ya Muingereza huyo kwa ajili ya kuimarisha eneo la kati huku ikielezwa kuwa huenda Xhaka na Partey wakaondoka.

Man City pia inatajwa kutaka kumsajili mchezaji huyo ambaye miezi 19 iliyopita alikataa ofa ya mkataba mpya West Ham ambao ungemfanya kulipwa pauni 200,000 kwa wiki.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button