Arsenal kwa Rice, Liverpool Danjuma

Arsenal imepeleka ofa kwa West Ham kutaka saini ya kiungo Declan Rice 24, baada ya kumkosa Mykhailo Mudryk aliyetimkia Chelsea. ( Times Subscription).

Mkurugenzi wa michezo wa Dortmund, Sebastian Kehl anakusudia kuanzisha mazungumzo na kiungo Jude Bellingham na wazazi wake juu ya mustakabali wake klabuni hapo. ( Kicker-in German ) Dortmund pia inataka kumsajili Elanga kutoka Manchester United ( Talksport).

Manchester United imeanzisha mazungumzo na Inter Milan na inataka kumsajili beki wa kulia, Denzel Dumfries, 26, United imepeleka £35m ofa hiyo inaendelea kujadiliwa (TuttoMercatoWeb – in Italian).

Raphina ambaye anatakiwa na Arsenal hana npango wa kuondoka Barcelona Januari hii ( Mundo Deportivo – in Spanish).

Newcastle United inaangalia uwezekano wa kumnasa kiungo Conor Gallagher, 22, na Ruben Loftus Cheek 26, na winga raia wa Morocco, Hakim Ziyech ( Telegraph Subscription).

Chelsea na Tottenham hawana mpango wa kumsajili Anthony Gordon 21 (CaughtOffside).

Tottenham na Liverpool ni miongoni mwa klabu zinazomfukuzia winga Arnaut Danjuma lakini Villarreal imepokea ofa kutoka Everton pekee( Relevo).

Beki wa Arsenal, William Saliba, 21, amesema ana furaha klabuni hapo hata hivyo mazungumzo ya kuongeza mkabata mpya yanaendelea. ( Independent) .

Juventus watajaribu kumsajili beki wa AS Roma, Chris Smalling, 33, kwa uhamisho huru ( Tuttosport)

Habari Zifananazo

Back to top button