LIGI Kuu nchini England inaendelea leo kwa michezo miwili, Arsenal itakuwa uwanja wa nyumbani Emirates kuikabili Everton na Liverpool itakuwa Anfield kuvaana na Wolver.
Mchezo wa Arsenal utaanza saa 4:45 usiku na utafuata wa Liverpool baada ya dakika 15. Michezo hiyo ni viporo ambapo Liverpool mpaka sasa ina michezo 23, Arsenal 24.
Arsenal inashika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi, wakati wapinzani wao Everton wakiwa nafasi ya 18.
Liverpool inashika nafasi ya saba, wapinzani wao Wolver wanashika nafasi ya 15 katika msimamo huo.