Arsenal presha inapanda, inashuka

LIGI Kuu nchini England inaendelea leo ambapo Arsenal itakuwa na kibarua kigumu cha kuikabili Liverpool katika Uwanja wa Anfiled, huku presha ikiwa kubwa kwa Arsenal kutokana na mbio za ubingwa kwa kuzingatia ushindi wa Man City jana.

Mchezo huo utapigwa saa 12:30 jioni. Kuelekea mchezo huo, beki wa Liverpool, Virgil van Dijk amepona na atarejea leo alikosa mchezo wa sare dhidi ya Chelsea.

Thiago Alcantara anaweza kurejea lakini Luis Diaz ana uwezekano mkubwa wa kurejea baada ya kupona goti aliloumia dhidi ya Leeds tarehe 17 Aprili.

Mchezaji wa Arsenal Bukayo Saka amepona homa iliyokuwa ikimsumbua na kufanya aanzie benchi wikendi iliyopita.

William Saliba na Eddie Nketiah hawatakuwa sehemu ya mchezo kwani bado hawajapona.

Liverpool wameshinda mechi sita zilizopita nyumbani dhidi ya Arsenal.

pharmacy

Arsenal hawajashinda katika mechi tisa za ugenini dhidi ya Liverpool. Walishinda mechi ya ligi mara ya mwisho Anfield mnamo 2012 wakati meneja wa sasa Mikel Arteta alipokuwa mchezaji wa timu hiyo.

Hii ni mara ya tisa kwa Arsenal kukutana na Liverpool kwenye EPL huku wakiwa vinara wa ligi (W3, D3, L2), huku michezo minane ya awali ikifikisha jumla ya mabao 33.

Habari Zifananazo

Back to top button