BAADA ya ofa ya pauni milioni 80 kukataliwa, Arsenal imeongeza dau hadi kufikia pauni milioni 100 kwa kiungo Declan Rice kutoka West Ham. Mtandao wa Sky Sport umeripoti.
Arsenal inataka kuimarisha eneo la kiungo, huku ikielezwa kuwa Rice atakwenda kuchukua nafasi ya Granit Xhaka ambaye taarifa zinasema huenda akajiunga na Bayer Levekusen ya Ujerumani.
The Gunners wamekuwa wakiisaka saini ya Mwingereza huyo kwa muda mrefu. Miezi 19 iliyopita Rice alikataa kuongeza mkataba ambao ungemfanya kulipwa pauni 200,000 kwa wiki.
Imeeripotiwa Manchester City wameanza vita na Arsenal ya kumsajili kiungo huyo ambaye pia anawindwa na Bayern Munchen.