Arsenal yakaa kileleni msimamo EPL

ARSENAL sasa imekaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England, baada ya sare ya bao 1-1 kati ya Liverpool na Manchester City.

‘The Gunners’ walishinda mchezo wao bao 2-1 dhidi ya Brentford jana, hivyo walikuwa wakisubiri mchezo wa leo City dhidi ya Liverpool.

Msimamo wa EPL unaonesha Arsenal inaongoza ligi kwa pointi 64 sawa la Liverpool tofauti ikiwa mabao ya kufunga na kufungwa.

Manchester City inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 63.

Habari Zifananazo

Back to top button