WAKATI dirisha la usajili nchini England likifungwa usiku wa leo, Arsenal inapambana kwa namna tofauti usajili wa wachezaji wa eneo la kiungo.
Baada ya Brighton kukataa kumuachia Moise Caicedo, Arsenal wamehamia kwa Jorginho kutoka Chelsea.
Imeelezwa mkabata wa Jorginho umebakia miezi sita, Chelsea wapo tayari kumuachia ila kwa dau kubwa.
Arsenal inatafuta kiungo ambaye atacheza kwenye eneo la Thomas Partey ambaye ubora wake na Sambi Lokonga kama mbadala wake umeachana mbali, huku Elneny akiwa majeruhi.
Awali timu hiyo yenye maskani yake London ilitaka kumsajili Declan Rice kutoka West Ham, dili hilo limeishia hewani na baada ya siku kadhaa Arsenal ikahamia kwa Caicedo.