Arsenal wanandaa ofa ya rekodi ya klabu ya pauni milioni 92 kumnunua kiungo wa kati wa West Ham,Declan Rice, 24. (Telegraph).
Wakati huohuo, kocha wa Arsenal, Mikel Arteta anafikiria kumsajili beki wa Manchester City na Ureno Joao Cancelo, 28, ambaye yuko kwa mkopo Bayern Munich, lakini The Gunners wanahofia kuwa City watasita kufanya biashara nao msimu huu wa joto. (TalkSport).
Kiungo wa kati wa Arsenal na Norway Martin Odegaard mwenye umri wa miaka 24, ambaye mkataba wake unamalizika 2025, anatazamiwa kusaini mkataba mpya. (90 Minutes).
Kiungo Albert Sambi Lokonga, 23, anaweza kuhamia Burnley kucheza chini ya meneja Vincent Kompany, ambaye alimfundisha Mbelgiji huyo katika klabu ya Anderlecht. (Express)