ARSENAL imetangaza kukamilisha usajili wa kiungo Declan Rice kutoka West Ham United kwa mkataba wa muda mrefu.
Rice amesaini mkataba wa miaka mitano utakaoisha Juni 2028, wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja.
Rice ametua Emirates kwa dau la pauni milioni 105, ameweka rekodi ya kuwa mchezaji Mwingereza mwenye gharama zaidi.
Arsenal sasa imekamilisha usajili wa wachezaji watatu, Kai Havertz kutoka Chelsea, Jurrien Timber kutoka Ajax na Rice.