Arsenal yamvutia kasi Rice

ARSENAL itaongeza kasi ya kumnunua Declan Rice kwa pauni milioni 92 kwa matumaini kwamba kiungo huyo wa kati wa West Ham na Uingereza, 24, anaweza kujiunga kwa wakati kwa ajili ya kuanza maandalizi mapya ya msimu ujao. Kwa mujibu wa mtandao wa Telegraph.

Kiungo huyo pia anawaniwa na klabu za Chelsea, Bayern Munchen na Manchester United.

Mwenyekiti wa West Ham United, David Sullivan amethibtisha jana kuwa nyota huyo ataondoka klabuni hapo, na kwamba baadhi ya timu zimeonesha nia ya kumtaka.

“Sio jambo tulilotaka litokee. Tulimpa pauni 200,000 kwa wiki miezi 18 iliyopita na alikataa. Huwezi kumbakisha mchezaji ambaye hataki kuwepo.” Alisema Sullivan.

Wakati huo huo West Ham wana nia ya kumleta kiungo mkabaji wa Fulham na Ureno, Joao Palhinha 27, kuchukua nafasi ya Rice.

Habari Zifananazo

Back to top button