Arsenal yapania kwa Gundogan

ARSENAL inakusudia kuongeza nguvu katika eneo la kiungo kwa kumchukua Ilkay Gundogan kutoka Manchester City ambaye mkataba wake unaisha msimu huu.

Mustakabali wa Gundogan kuhusu mkataba mpya bado haujajulikana hivyo endapo hatopewa mkataba mpya Mjerumani huyo ataondoka bure.

Licha ya kuwindwa na Arteta ambaye aliwahi kufanya naye kazi Man City kama kocha msaidizi, pia Gundogan anawindwa na Barcelona, kwa kujibu wa Gazeti la The Guardian la Uingereza.

Arsenal pia imewahi kusajili wachezaji wawili kutoka City, Gabriel Jesus na Alexander Zinchenko.

Habari Zifananazo

Back to top button