Arsenal yatambulisha uzi mpya

KLABU ya Arsenal imetambulisha jezi zao mpya zitakazotumika   msimu wa Ligi Kuu England 2023/2024.

Kampuni ya utengenezaji vifaa vya michezo, Adidas inaendelea kutengeneza jezi hizo, ambapo mkataba wao na Arsenal wa pauni milioni 300 unamaliza mwaka 2030.

Shirika la ndege la Serikali ya Dubai, Fly Emirates pia wanaendelea kuwa wadhamini wakuu wa timu hiyo kwenye sehemu ya mbele ya jezi hizo.

Mkataba wa Arsenal na Emirates unaisha msimu ujao. Sehemu hizo mbili zilianza ushirikiano wa kibiashara mwaka 2006, kabla ya 2018 kusaini mkataba mpya wa pauni milioni 200. Takribani miaka 18 sasa tangu wameanza biashara hiyo.

Hata hivyo, Serikali ya Rwanda inaendelea kutangaza utalii wao kwa kuweka maneno ya ‘Visit Rwanda’ kwenye bega la kushoto la jezi hizo.

Arsenal imetoa jezi za nyumbani bado za ugenini mbili. Mpaka sasa ni Arsenal, Liverpool na Manchester City ndizo zimetoa uzi wao mpya wa msimu wa 2023/2024.

Habari Zifananazo

Back to top button