GAZETI la The Guardian nchini Uingereza limeripoti kuwa Arsenal inakaribia kumnasa kiungo, Declan Rice kwa dau la pauni milioni 100.
Wakati taarifa hizo zikishika kasi miongoni mwa vyombo vya habari, taarifa kutoka nchini Ujerumani zinaeleza kuwa Bayern Munchen wanamfuatilia kwa ukaribu.
Miezi 18 iliyopita Rice alikataa kusaini mkataba mpya ambao ungemfanya kuchukua mshahara wa pauni 200,000. Kwa wiki huku uongozi wa West Ham ukifanya juhudi za kumbakisha.
Vita ya Arsenal na Bayern inaendelea na hivi karibuni itathibitika atakayeshinda mchuano wa kumgombania nyota huyo.