Arsenal yaweka £105m kwa Rice

VITA ya Arsenal na Man City kwa Declan Rice inaendelea kushika kasi baada ya ‘The Gunners’ kuwasilisha kwa West Ham £100m ikiwemo £5m ya nyongeza endapo usajili utakamilika.

City jana waliweka mezani £80m pamoja na £10m ya nyongeza hata hivyo West Ham waliikataa ofa hiyo.

Ofay ya City ilikuja baada ya West Ham kukataa £75m na nyongeza ya £15m kutoka Arsenal.

Advertisement

West Ham sasa wanasubiri City kuona kama itapanda dau kwa Muingereza huyo.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *