Arteta anautaka ubingwa
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesema timu hiyo bado ina nafasi ya kushinda ubingwa msimu huu.
Timu hiyo jana ilipoteza kwa mabao 3-1 dhidi ya Man City na kushushwa hadi nafasi ya pili.
Kupoteza kwa Arsenal kumeipa City nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa EPL ikiongoza kwa pointi 51 sawa na Arsenal, City inaongoza kwa tofauti ya mabao.
pharmacy
“Bado wana imani, mimi pia nahisi ubingwa, wanahisi kabisa wanaweza kutwaa.” Amesema Arteta.
Baada ya kuifunga Manchester United Januari 22, Arsenal ilikuwa juu kwa tofauti ya pointi tano dhidi ya City ikiwa na mchezo mmoja mkononi, lakini mpaka sasa imepata pointi moja tu katika tisa.