Arteta: Jesus bado kidogo

KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amesema matarajio ya kurejea uwanjani kwa mshambuliaji Gabriel Jesus “hayupo mbali ila yupo mbali kurejea” Arteta amesema wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kesho wa EPL dhidi ya Bournemouth.

Mshambuliaji huyo raia wa Brazil aliumia akiwa na timu yake ya taifa katika michuano ya Kombe la Dunia lililofanyika nchini Qatar 2022. Mchezaji huyo ameanza kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza.

Arteta amezungumzia hali ya mshambuliaji mwingine, Eddie Nketiah ambapo amesema “tunampima na kuona mwelekeo wake”. Kuhusu kiungo Jorginho: “Jorginho yuko sawa, alikuwa na ugonjwa”. Ameongeza Arteta.

Timu hiyo itacheza mchezo wa raundi ya 26 dhidi ya Bournemouth katika uwanja wao wa nyumbani Emirates saa 12:00 jioni.

Habari Zifananazo

Back to top button