Arteta kocha bora Februari

KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amechaguliwa kuwa meneja bora wa Mwezi Februari 2024 wa Ligi Kuu nchini England akishinda kwa mara ya saba.

Arsenal ya Arteta ndiyo timu pekee ya Ligi Kuu iliyopata rekodi ya kushinda kwa asilimia 100 mwezi Februari, ikiwashinda vinara Liverpool, West Ham United, Burnley na Newcastle United.

The Gunners pia walikuwa na safu ya ushambuliaji bora zaidi, wakifunga mabao 18.

Habari Zifananazo

Back to top button