Arusha imependeza

UWEKAJI wa taa za barabarani mkoani Arusha na baadhi ya wilaya zake umepelekea mandhari ya maeneo husika kuwa na mwanga zaidi ikiwemo wapenda mazoezi ya viungo kuongeza muda zaidi wa mazoezi yao nyakati za usiku na watalii

Akizungumzia mafanikio ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Hassan Suluhu, Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Arusha, Mhandisi Reginald Massawe amesema uwekaji wa taa za barabarani unaotekelezwa na Tanroads umewezesha madhari ya miji kuwa mazuri ikiwemo usalama kwa raia na watalii hususan wale wanaopenda kufanya mazoezi ya mwili kuongeza muda zaidi wa mazoezi yao.

“Tumeweka taa za barabarani katika mji wa Longido,Mto wa Mbu, Karatu,Arusha Mjini hadi Kisongo na tutaendelea na zoezi la uwekaji taa za barabarani kwenye maeneo mbalimbimbali ya Mkoa wa Arusha ili watu wanaofanya biashara za kujikwamua kiuchumi waweze kuuza”

Lakini pia katika kipindi cha miaka mitatu Tanroads Mkoani Arusha imetengewa Sh,bilioni 49 kwa miradi ya matengenezo ya baraba ikiwemo Sh bilioni 1.3 kwa kazi za dharura zilizotoka na matengenezo ya barabara na madaraja.

Habari Zifananazo

Back to top button